Home Michezo Manji ahofia Yanga kuchafuka kwa dawa za kulevya

Manji ahofia Yanga kuchafuka kwa dawa za kulevya

19
0

Baada ya jina lake kutajwa miongoni mwa watu wanaohusishwa na madawa ya kulevya, Mwenyekiti wa Yanga Yusuf Manji ameibuka na kusema, unapozungumza jambo la kumchafua yeye kama Mwenyekiti wa Yanga ni sawa na kuichafua Yanga nzima.

Manji alikutana na waandishi wa habari saa chache baada ya jina lake kutajwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam akituhumiwa kuhusika na dawa za kulevya ambapo Manji alisema jina lake kutajwa kwenye vyombo vya habari akituhumiwa kuhusika na dawa za kulevya ni kuhatarisha maisha yake.

“Ukinihusisha na jambo chafu hata kama nia yako ni kusafisha umenichafua mimi na wakati unanichafua mimi kama Mwenyekiti wa Yanga, unachafua Yanga nzima, ukichafua Yanga nzima maana yake watu milioni 30 wanachafuka,” amesema Manji wakati akizungumza na waandishi wa habari.

“Kusimamia taasisi yenye mamilioni ya watu na kuhakikisha kuna amani, utulivu na maendeleo pamoja na changamoto zote zilizopo halafu bado nikawa nashughulika na dawa za kulevya basi nitakuwa Mungu mtu.”

“Kama unataka mimi nikusaidie kwenye vita yako na vita ya nchi kuhusu dawa za kulevya, ukinitangaza unaweka maisha yangu kwenye hatari.”

“Nia ya kunitangaza kwenye vyombo vya habari kunaweza kuwa na sababu tatu; natumia dawa za kulevya, nauza au unataka mimi niuawe.”