Home Michezo Manula aumia, Bocco ashindwa kujiunga na kikosi kwaa ajili ya maandalizi

Manula aumia, Bocco ashindwa kujiunga na kikosi kwaa ajili ya maandalizi

345
0

Djibouti City.
Simba itamkosa nahodha wake Jonh Bocco, na kipa wake Aishi Manula anayejitonesha katika mazoezi ya leo jioni Jumatatu.

Bocco aliumia wakati wa mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Mwadui alikwenda safari hiyo, pigo kubwa kwa Simba ni kuumia kwa kipa wake tegemeo Manula.

Simba itacheza mechi yake ya marudiano ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Gendarmarie ya Djibouti kwenye Uwanja wa State de Vile wenye uwezo wa kuingia mashabiki 40,000.

Simba iliwasili nchini Djibouti usiku wa saa nane kuamkia leo, Jumatatu ukiwa na matumaini makubwa ya kuibuka na ushindi.

Lakini wasiwasi ni kwa hao wachezaji wawili Bocco anasumbuliwa na enka na Aishi ameshtua kidole cha mkono.

Pia kwa upande wa uongozi, Kocha msaidizi wa Simba, Masoud Djuma amesema kila kitu kinakwenda sawa.