Marafiki wa Aguero wanajua kuwa anaondoka. - The Choice

Marafiki wa Aguero wanajua kuwa anaondoka.

0

Hali sio nzuri kabisa kwa mshambuliaji wa Man City na timu ya taifa ya Argentina Sergio Aguero.Aguero amekuwa na wakati mgumu Man City toka kuwasili kwa nyota mpya wa Brazil Gabriel Jesus.Kiwango anachoonesha Jesus kimemshawishi kocha wa City Pep Gurdiola kumuanzisha yeye huku Aguero akianzia benchi jambo ambalo Aguero anaona ni kukosewa heshima.

Aguero sasa amewaambia rafiki zake kuhusu mpango wake wa kuondoka City.Kocha Pep anaonekana imani yake kwa Aguero pamoja na kuwa mfungaji hatari misimu miwili mfululizo imepungua.Gurdiola anaona Aguero sio mzuri sana katika mfumo wake kama ilivyo kwa Jesus.Jesus ambae haikuchukua muda mrefu toka asajiliwe City kwani mechi 3 tu za mwanzo alionesha nini kimemleta City.
Wiki iliyopita Aguero aliulizwa kuhusu mkataba wake na Man City unaisha mwaka 2020.Katika mazungumzo yake Aguero anaonekana yeye mwenyewe ni kama haamini kama atafikisha 2020.“Sijui kuhusu huko mbeleni lakini timu ndio itakayoamua kama inanihitaji au laa,nina miezi mitatu ya kuonesha kile nilichonacho lakini baada ya msimu klabu ndio itakayoamua” alisema Aguero.
Pamoja na Aguero kusema kwamba timu ndio itamuamulia lakini watu wake wa pembeni tayari wanajua kwamba Kun anaondoka.Chanzo kimoja cha karibu na Aguero kilisema “Aguero sio mvivu,anafanya kazi kwa bidii sana lakini kocha Pep anadai haendani nae na jambo hili linamuumiza sana Kun”.
Tayari Chelsea,Inter Millan na Real Madrid wameshaanza kufungua milango kwa ajili ya Aguero.Chelsea wenyewe bado hawaamini kama Diego Costa atabaki nao msimu ujao naada ya matajiri wa China kuanza kumgusa gusa lakini hata akibaki bafo Chelsea wanahitaji striker wa kumpa changamoto Costa na Aguero anaonekana mtu sahihi kwao.
Share.

About Author