Home Michezo MASKINI…Baada ya Kunyimwa Dhamana JAMAL Malinzi Apata Pigo Jingine Akiwa Jela

MASKINI…Baada ya Kunyimwa Dhamana JAMAL Malinzi Apata Pigo Jingine Akiwa Jela

192
0

Viongozi wa ngazi ya juu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) huenda wanaoshitakiwa kwa jumla ya makosa 28 huenda wakawa katika wakati mgumu baada ya wakili wa kujitegemea, Jerome Mswemwa aliyekuwa anawawakilisha, kujitoa rasmi.

Msemwa alikuwa akiwawakilisha Rais wa TFF, Jamal Malinzi, Katibu MKuu wa TFF, Selestine Mwesigwa na  Mhasibu wa TFF, Nsiande Mwanga katika kesi namba 213 ya mwaka 2017.

Kielezea uamuzi wake wa kujiuzulu kupitia barua aliyoandika kwenda kwa Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu, Wilbard Mashauri, Msemwa alisema ameomba kujiondoa katika kesi hiyo baada ya kutokuopewa taarifa sahihi kutoka kwa wateja wake anaowawakilisha.

Jamal Malinzi (57), Katibu Mkuu wake, Mwesigwa Celestine (46) na Mhasibu, Nsiande Mwanga (27) walipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka mbalimbali ikiwamo ya kughushi na kutakatisha fedha dola za Marekani 375,418 (Sh840 milioni).