Home Michezo Mayanja amezungumzia kuhusu Simba kushinda mfululizo

Mayanja amezungumzia kuhusu Simba kushinda mfululizo

15
0

Zainabu Rajabu

KOCHA msaidizi wa timu ya Simba Jackson Mayanja amesema anawapongeza wachezaji wake baada ya kupata ushindi dhidi ya African Lyon na kutinga robo fainali ya michuano ya  kombe la shirikisho.

Simba imekuwa timu ya Kwanza kutinga robo fainali huku ikisuburi ipangiwe itacheza na nani katika  hatua ya robo fainali.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo  kocha msaidizi Jackson Mayanja amesema mchezo ulikuwa mgumu na waushindani huku kila moja akitaka kupambana ili kusonga mbele katika hatua inayofata.

“Nafurahi sana kuona vijana wangu wanavyojituma na kusikiliza kile tunachowafundisha mazoezini, ndiyo kinachopelekea sisi kushinda mechi takribani nne bila kufungwa,” alisema Mayanja.

Simba inatarajia kuondoka kesho majira ya asubuhi kuelekea kisiwani Unguja kwa ajili ya kuweka kambi ya wiki moja kabla ya kukutana  na watani zao (Yanga).