Home News Mbunge iteko achangia miradi ya maendeleo Jimboni Bukombe

Mbunge iteko achangia miradi ya maendeleo Jimboni Bukombe

1286
0
Na George Binagi-GB Pazzo
Mbunge wa Jimbo la Bukombe mkoani Geita, Doto Biteko (CCM), ameunga mkono juhudi za maendeleo za wakazi wa Kata ya Namonge jimboni humo kwa kuchangia utekelezaji wa miradi ya maendeleo iliyoanzishwa na wakazi hao.
Akizunguma kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Shilabela Novemba 03, 2018, Biteko ambaye pia ni Naibu Waziri wa Madini alichangia mifuko 30 ya saruji kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa choo katika Shule ya Msingi Shilabela pamoja na shilingi laki nane kwa ajili ya ujenzi wa choo katika Shule ya Msingi Nyamagwangala.
Biteko alitumia mkutano huo kuwapongeza wananchi wa Jimbo la Bukombe kwa kubuni na kutekeleza miradi mbalimbali ya ya maendeleo na kwamba serikali itaendelea kuwaunga mkono kwani maendeleo ni ushirika baina ya serikali na wananchi.
Mbunge wa Jimbo la Bukombe mkoani Geita, Doto Biteko (CCM) ambaye pia ni Naibu Waziri wa Madini, akizungumza na wakazi wa Kata ya Namonge kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji cha Shilabela.