Mbunge Zitto Kabwe awaambia waandishi kutoandika habari zozote za Serikali hadi serikali ifanye haya

0

ZITTO

Mkuu wa Mkoa anavamia chumba cha habari binafsi Kwa mitutu ya Bunduki na Askari wa Umma. Wananchi wanalalamika kuhusu uvamizi huu ikiwemo Waziri, Wabunge, Wamiliki Wa vyombo vya habari na waandishi wenyewe.
Rais bila kumung’unya maneno anatamka hadharani kuwa Mkuu wa Mkoa aendelee na kazi zake. Hii maana yake ni kwamba Rais amemtuma Mkuu wa Mkoa kuvamia Chombo cha habari.
Nawashauri wana habari wote kukutana kupitia MOAT, Jukwaa la Wahariri na Press Clubs na kuamua Kwa pamoja kususia kuandika habari zote za Serikali mpaka hapo Serikali 1) itakapolaani tukio hili na kuahidi kuwa halitotokea tena 2) itakapochukua hatua kali dhidi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam.

Nakumbuka Sana Jukwaa la Wahariri chini ya Sakina Dewji-Datoo

Screenshot_20170320-152239

Facebook Comments
Share.

About Author