Home Michezo Mchezaji huyu wa Man united kufungwa miaka minne Jela

Mchezaji huyu wa Man united kufungwa miaka minne Jela

119
0

Kulikuwa na kesi ambayo ilikuwa ikiihusisha klabu ya zamani ya kiungo wa Manchester United Zaragoza ambapo May mwaka 2011 walihusishwa na kupanga matokeo pamoja na klabu ya Levante.

Kesi kuhusu tukio hilo ilikuwa bado inaendelea nchini Hispania lakini sasa mawakili wanaosimamia kesi hiyo wameibuka na kuitaka mahakama kutoa hukumu ya miaka 4 jela kwa wahusika wa kesi hiyo.

Mara nyingi kesi za watu maarufu nchini Hispania huwa chini ya miaka 2 hali inayowapelekea kutumikia kifungo nje ya gereza lakini sasa kwa Ander Herrera upande wa washtaki umependekeza kutolewe adhabu ya miaka 4 gerezani.

Sio tu kwenda jela miaka 4 lakini pia mahakama imetakiwa kutoa adhabu ya kutojihusisha soka kwa miaka 6 baada ya kutoka jela kwa Herrera pamona na wenzake 35 ambao walihusika katika tukio hilo.

Ushindi wa Zaragoza wa mabao 2 kwa 1 vs Levante mwaka 2011 uliwafanya Derpotivo La Coruna kushuka daraja matokeo ambayo baadae iligundulika kwamba Levante na Zaragoza walipanga matokeo.

Pia Herrera na wenzake wanatakiwa kutoa faini £2.9m kila mmoja, wachezaji wengin