Home Michezo .Mchezaji Samatta Aumia Pua Mchezoni..Anasubiri Vipimo Kujua Kama Pua Imevunjika

.Mchezaji Samatta Aumia Pua Mchezoni..Anasubiri Vipimo Kujua Kama Pua Imevunjika

59
0

Jumapili April 24 usiku timu ya Genk ilishuka dimbani kuchuana na Gent lakini taarifa mbaya kuhusu star wa Bongo kwenye ligi ya Ubelgiji Mbwana Samatta ni kwamba, amepata majeraha katika mchezo huo ambao alianza kwenye kikosi cha kwanza lakini hakuweza kumaliza dakika zote 90.

Kipindi cha pili Samatta alishindwa kurudi uwanjani kuendelea na mchezo kutokana na maumivu aliyoyapata kipindi cha kwanza baada ya kugongwa pua. Ilibidi nafasi yake ichukuliwe na Nikolaos Karelis aliyeingia dakika ya 46 kipindi cha pili.

Timu ya Genk imepoteza mchezo wake wa Jupiter League baada ya kukubali kipigo cha 2-1 vs Gent.