Home Uncategorized MCHUNGAJI MASHIMO ATOA SIKU SABA WABAYA WA WEMA KUOMBA RADHI

MCHUNGAJI MASHIMO ATOA SIKU SABA WABAYA WA WEMA KUOMBA RADHI

1282
0

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

MCHUNGAJI wa Mitume na Manabii na Maaskofu Tanzania wa kanisa la Emmaus Bible Church Pentecostal Komando Mashimo ametoa siku saba kwa maadui wa Msanii wa Filamu nchini Wema Sepetu kumuomba radhi kwa mabaya waliyomfanyia.

 

Mchungaji wa Mitume na Manabii na Maaskofu Tanzania wa kanisa la Emmaus Bible Church Pentecostal Komando Mashimo akizungumza na waandishi wa habari (hapo pichani) jijini Dar es Salaam.

Mashimo alisema hayo leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo ameeleza kwamba kama wasipo fanya hivyo atafanya ibada ya majeneza dhidi yao ili kuwazika.

“Natoa siku saba wale maadui wa wema wakamuombe radhi, baada ya siku saba nitafanya ibada ya majeneza ya kuwazika maadui wa Wema,” alisema Mchungaji Mashimo.

Alibainisha kuwa maadui wa Wema wapo Saba na ndio waliopo nyuma ya mtua aliyedaiwa kuwa mchumba wake hivyo watu hao ndio walimtumia kama mtego kwa Msanii huyo kwani ndiye aliyevujisha video zao kenye mitandao ya kijamii.

“Ni kwamba zile video hakutuma Wema, bali ni yule mchumba wake na alifanya hivyo kwa kutumiwa na alikuwa akilipwa pesa kwa kufanya vile,” alisema.

Mashimo alitoa wito kwa Watanzania kumuheshimu Miss Tanzania huyo wa zamani na kuwataka wajue kuwa Wema ni mtumishi na mtoto wa Mungu hivyo asichukuliwe kama mtenda maovu kuliko wao kwani kuna hata Manabii na Maaskofu ambao ni waovu pia.

Kutokana na Wema kukabiliwa na maadui hao Mchungaji Mashimo ameandaa ibada ya Maombi kwa ajili yake itakayofanyika Jumamosi ya Novemba 10, 2018 kuanzia saa 4 asubuhi.