Home Michezo Mechi la Juve na Madrid Kuchezwa Huku Paa la Uwanja Likiwa Limefungwa...

Mechi la Juve na Madrid Kuchezwa Huku Paa la Uwanja Likiwa Limefungwa Kuhofia Mabomu ya Kujitoa Muhanga ya Islamic State

13
0
 Paa la Uwanja wa Taifa wa Wales litafungwa kwa sababu za kiusalama wakati wa fainali ya Ligi ya Mabingwa itakayofanyika mjini Cardiff.
Mashabiki wanaokadiliwa kufikia 170,000 wanategemewa kusafiri na kushudia mechi hiyo dhidi ya Real Madrid hapo Juni 3.
Itakuwa ni mechi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa kuchezwa kwenye uwanja huku paa lake likiwa limefungwa.
Shirikisho la Soka la Wales (FAW) limesema usalama ndiyo kipaombele chao cha kwanza.
Paa litafungwa kwa sababu ya kuhofia mashambulia ya drone kwa kile kinachotokea kunapofanyika mechi kubwa duniani.