Home Michezo MECHI YA SIMBA NA YANGA YAMVUTA LOWASSA UWANJA TAIFA

MECHI YA SIMBA NA YANGA YAMVUTA LOWASSA UWANJA TAIFA

20
0

Waziri Mkuu aliyejiuzuru  na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa anatarajiwa kuwa miongoni mwa maelfu ya mashabiki watakaohudhuria pambano la watani wa jadi  Simba na Yanga linalotarajiwa kufanyika mapema hii leo kwenye uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam.

Simba inaikaribisha Yanga leo katika pambano la Ligi Kuu Tanzania (VPL) ambapo kuelekea mechi hiyo, Lowassa aliyekuwa Mgombea Urais wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015, kupitia Ukawa anatarajiwa kushuhudia pambano hilo.

Aidha Lowassa amewaonya waamuzi waliopewa dhamana ya kuchezesha mechi hiyo, kutenda haki na si vinginevyo ambavyo imezoeleka.

“Nakwenda uwanjani kutazama mechi ya watani wa jadi, lakini mtu yeyote akitaka kujua kama mimi ni shabiki wa timu gani basi aje uwanjani, ataniona na kuelewa nashabikia timu ipi,”amesema Lowassa.

Hata hivyo, amesema kuwa ataingia mapema uwanjani hapo lakini pia atatumia fursa hiyo kutegua kitendawili cha muda mrefu cha timu ipi anaishabikia  kati ya Simba na Yanga.