Home Michezo Mgombea urais TFF ambiwa si raia wa Tanzania

Mgombea urais TFF ambiwa si raia wa Tanzania

127
0
Mgombea wa urais wa TFF Wallace Karia amethibitisha kuwekewa pingamizi kwamba si raia wa Tanzania hivyo hana sifa za kugombea kwenye uchaguzi mkuu wa TFF unaotarajia kufanyika Agosti 12, 2017.
“Nimewekewa pingamizi nimeambiwa kwamba sio raia wa Tanzania, nimeingia ndani nimeonesha vyeti vyangu vya kuzaliwa, passport zangu na maelezo yangu nimeyatoa baada ya mlalamikaji kusema mimi sio raia wa Tanzania lakini hakuwa na kielelezo chochote.”
“Ametoa maelezo ya mdomo kwamba aliambiwa na baba yake kwamba baba yangu alikuwa sio raia wa Tanzania na akataja jina ambalo sio mzee Mohamed alifariki na kuzikwa Somalia.”
“Nikawauliza wajumbe kwa nini wamepokea pingamizi ambalo halina uthibitisha rasmi huku pingamizi hilo likiwa ni la mdomo, lakini wajumbe wameendelea kusisitiza kwamba wanataka wafanye mawasiliano na taasisi ya uhamiaji kujua kama mimi ni raia au si raia wa Tanzania.”
“Nimewaonya kwamba, kama huu utakuwa ni uongo ni vizuri mlalamikaji akachukuliwa hatua ikiwa ni pamoja na kupelekwa kamati ya maadili endapo itathibitika kama mimi ni raia wa Tanzania.”
“Baba yangu ana asili ya Somalia lakini baba yangu ni mtanzania, amefariki lakini tulimzika hapahapa.”
Karia amesema yeye ni mzaliwa mkoa wa Tanga, alizaliwa mwaka 1963 kwenye hospitali ya Galanosi amepata elimu yake Tanga hadi kidato cha nne kisha badae akaendelea kidatato cha tano kabla ya kupata taaluma ya uhasibu kwenye chuo cha uhasibu DSA wakati huo sasa hivi ni Taasisi ya uhasibu.
Amesoma pia chuo cha usimamizi wa fedha na chuo cha uhasibu Arusha kisha akaenda kusoma shahada ya pili Coventry University England. Kwa sasa Karia ni mtumishi wa serikali kwenye ofisi ya mkuu wa mkoa Morogoro.