Home Mahusiano Miss Universe Tanzania Kujenga Uelewa na Utetezi Kwa Watoto

Miss Universe Tanzania Kujenga Uelewa na Utetezi Kwa Watoto

278
0

Mkufunzi kutoka CCBRT, Dr. Nancy Lwezimula akifundisha jambo kuhusu mdomo sungura.

NO-2

Miss Universe Tanzania 2015, Lorraine Marriot akicheza na mtoto  Jeremia Athuman mwenye tatizo la mdomo sungura.

NO-3

Lorraine Marriot Miss Universe Tanzania 2015, akifurahi pamoja na mtoto Jeremia Athuman.

NO-4

Miss Universe Lorraine akiwa na mtoto mwenye mdomo sungura.

NO-5

Miss Universe katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo wa juu ya uasuaji wa watoto wenye tatizo la mdomo sungura. Wa kwanza kutoka kulia kwenda kushoto mbele ni Erwin Telemans Mkurugenzi Mtendaji-CCBRT, akifuatiwa na  Miss Universe Tanzania 2015, Lorraine Marriot , Ian B. Walker – Mkurugenzi wa uraia, Conrad Person-Mkurugenzi, Africa Region Corporate Contribution pamoja na wadau wengine.

Miss Universe Tanzania ameungana na Smile Train Afrka kujenga uelewa na utetezi kwa watoto wenye mdomo sungura.

SmileTrain ni shirika la kimataifa linalosaidia  watoto pamoja na mbinu endelevu ikiwemo ya kutatua tatizo la mdomo sungura. Mamilioni ya watoto katika nchi zinazoendelea wanaoishi na tatizo la midomo sungura (Mdomo wazi) bila kutibiwa wanaishi kwa kutengwa, lakini muhimu zaidi, hupata ugumu katika kula , kupumua na kuzungumza. Upasuaji wa midomo yenye uwazi (ufa)  ni rahisi, na huleta mabadiliko ya haraka.

Kupitia ushirikiano huu, Miss Universe Tanzania mwaka 2015, Lorraine Marriot ni Balozi wa Nia Njema wa Smile Train nchini Tanzania na anasaidia  kuongeza uelewa wa masuala ya watoto wanaoishi na tatizo la mdomo sungura. Jana, Aprili 22, 2016, Lorraine alihudhuria mafunzo kwa ‘mabalozi wapya’ juu ya utambulisho na rufaa za wagonjwa wenye midomo sungura katika hospitali ya CCBRT, ambayo ni moja ya hospitali wanaoshirikiana na Smile Train. Mafunzo haya yamewezeshwa kwa ufadhili wa Vodafone Foundation na  USAID / PEPFAR kupitia Public Private Partnership.

Smile Train inatoa mafunzo endelevu, fedha na rasilimali ili kuwawezesha madaktari wa ndani katika nchi zaidi ya 85 zinazoendelea kutoa 100% – katika upasuaji na ukarabati katika jamii zao wenyewe. Hadi sasa, washirika wa ndani wa Smile Train nchini Tanzania wamesaidia zaidi ya watoto 5,000 na wanafanya kazi katika mikoa ya Arusha, Mwanza, Tanga na Dar es Salaam. Aidha, karibu watoto 1,700 nchini Tanzania huzaliwa na tatizo la mdomo sungura kila mwaka.

Smile Train hutoa msaada wa kifedha ili kusaidia kufidia gharama kwa ajili ya upasuaji na pia imetoa msaada kwa ajili ya vifaa muhimu na salama kama oximeters na vifaa vya upasuaji   na kusambaza vifaa kama visu na uzi wa mishono. Uwekezaji wote huu si tu kwamba unawezesha upasuaji mkubwa lakini pia unafanya upasuaji huu uwe salama na wa ubora wa hali ya juu.