Home News MJUE MSANII MPYA CHIPUKIZI WA BONGO FLEVA WA DK. SHIKA

MJUE MSANII MPYA CHIPUKIZI WA BONGO FLEVA WA DK. SHIKA

1683
0

 

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Bilionea wa Nyumba za Lugumi Dk. Luis Shika leo amemtambulisha Msanii Chipukizi wa Muziki wa Kizazi Kipya maarufu kama ‘Bongo fleva’ Salim Magembe ‘K.L.O.H’ ambaye atakuwa chini yake.

Akizungumza na vyombo vya habari alipokuwa akimtambulisha msanii huyo, Dk. Shika alisema sababu za kumchukua msanii huyo ni kutokana na kuwa na sauti nzuri, uwezo mzuri wa kuimba na mwonekano wa kisanii.

Aliongeza kuwa msanii huyo ana uwezo mzuri wa kutunga mashairi yenye kuendana na rika mbalimbali pamoja na kuwa na maadili.

“Kwa hiyo nategemea kwamba rika zote zitafurahia nyimbo zake, niwaombe watanzania muwe na amani mtafurahia na hivi karibuni naandaa uwezekano wa kwenda naye nje kufanya video,” alisema Dk. Shika.

Aidha alitangaza kazi kwa waandaaji wa muziki kwani anatarajia kuanzisha Lable yake ya Musiki itakayojulikana kama ‘Shika Music Lable”

Kwa upande wake Msanii huyo alisema kuwa hadi sasa ananyimbo za audio zaidi ya 30 na video mbili ambapo miungoni mwa nyimbo hizo amewashirikisha wasanii wakongwa kama P.N.C na Country Boy.

“Mimi ni msanii chipukizi niliyeanza muziki miaka miwili iliyopita na nimeweza kufanya kazi kadhaa, nina audio zaidi ya 30 na video mbili, video moja nilifanya mwaka jana niliyomshirikisha P.N.C lakini haikuweza kufika popote kutokana na kokusa fedha,” alisema Magembe.

Magembe alisema kwamba kuwa chini ya Dk. Shika kutamsaidia kufanya kazi zake vizuri na kueleza kuwa hadi sasa wamekwisha panga mipango ya namna ya kufanya kazi.

Aliomba ushirikiano kwa watanzania na kuwaahidi kuwa watarajie burudani nzuri ya musiki kutoka kwake.