MSAFARA WA RUVU SHOOTING WAPATA AJALI, TAIRI LAPASUKA SAFARINI - The Choice

MSAFARA WA RUVU SHOOTING WAPATA AJALI, TAIRI LAPASUKA SAFARINI

0

Taarifa ni kuwa msafara wa timu ya Ruvu Shooting umeripotiwa kupata ajali mbele Kidogo ya Singida wakiwa safarini kurejea Dar es Salaam.

Habari ambazo zimethibitishwa na mmoja wa wachezaji wa timu hiyo zimeeleza kuwa gari likiwa katika mwendo wa kasi kiasi ndipo tairi likapasuka na kusababisha gari kuhama njia na kuparamia miti iliyokuwa jirani.

Imeelezwa kuwa hakuna mtu yeyote aliyepata majeraha makubwa katika tukio hilo, isipokuwa mchezaji mmoja ambaye amepata majeraha ya kawaida.

Timu hiyo ilikuwa mkoani Shinyanga ilipocheza mechi ya mwisho ya Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2016/17 dhidi ya Stand United na kupoteza kwa mabao 2-1 lakini timu hiyo imebaki ligi kuu kwa kushika nafasi ya saba.

Alipoulizwa Ofisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire alisema ni kweli ajali hiyo imetokea wakiwa njia Manyoni Singida mita 200 kuacha njia panda ya Itigi.
Gari ilipopata ajali iliacha njia kama mita 400 kutoka barabarani iliyosababishwa na taili ya mbele kupasuka.
Wachezaji watatu wameumia pamoja na yeye Masau Bwire wa nne. Wachezaji walioumia ni Yussuf Nguya, Abdul Mpambika na Saidi Dilunga.

Facebook Comments
Share.

About Author