Mshambuliaji wa Simba auza Dukani South baada ya kukosa Timu ya kuichezea

0

STRAIKA WA SIMBA AUZA DUKA SAUZI

HII inahuzunisha kidogo. Unamkumbuka yule mshambuliaji wa Simba, Hija Ugando? Kwa sasa yupo Afrika Kusini akiuza duka baada ya kukosa timu ya kuichezea nchini humo.

Ugando aliomba kuachwa na Simba mwaka jana kwa madai kwamba amekuwa hapati nafasi ya kucheza klabuni hapo lakini maisha ni kama yamekwenda kinyume na matarajio yake sasa.

Ugando alisema kwamba alienda nchini humo kwaajili ya kufanya majaribio ili apate timu, lakini mambo yamemwendea tofauti hivyo kujikita kwenye kazi hiyo ya dukani. “Nilikuja kwaajili ya kufanya majaribio lakini bado sijapata timu mpaka sasa, nimeamua kugeukia kazi hii ya kuuza duka ili mambo mengine yaweze kwenda,” alisema.

Akizungumzia kuhusu maisha yake nchini humo, alisema anaishi katika nyumba ya bosi wake ambaye anamuuzia duka, lakini hajakacha kabisa mpira kwani anafanya mazoezi na Watanzania waliopo nchini humo.

3,093 total views, 2 views today

Facebook Comments
Share.

About Author