Home Michezo MSIBA: Mchezaji wa zamani wa Yanga na Taifa Stars amefariki dunia

MSIBA: Mchezaji wa zamani wa Yanga na Taifa Stars amefariki dunia

13
0

Godfrey Bonny kiungo wa zamai wa klabu ya Yanga na timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ amefariki dunia alfajiri ya leo huko nyumbani kwao Mbeya.

February 2, 2017 mtandao huu uliandika habari ya kuumwa kwa Godfrey Bonny ambaye alikuwa amelazwa hospitali ya Rungwe-Tukuyu Mbeya alikokuwa akipatiwa matibabu.

Wakati akicheza soka, Bonny aliwahi kuvitumikia vilabu vya Tanzania Prisons na Yanga kwa vipindi tofauti pamoja na timu ya taifa ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’.

shaffihdauda.co.tz inaungana na wadau wengine wa soka na michezo kwa ujumla, kutoa pole kwa familia ya Godfrey Bonny kwenye kipindi hiki kigumu cha msiba wa mpendwa wetu.

R.I.P Godfrey Bonny, hakika tutaendelea kukumbuka kile ulichokifanya katika soka la Tanzania.