Home Michezo Msuva akunwa na Uwezo wa mchezaji huyu wa Simba,Amtabiria Kimataifa

Msuva akunwa na Uwezo wa mchezaji huyu wa Simba,Amtabiria Kimataifa

116
0

Msuva akunwa na Uwezo wa mchezaji huyu wa Simba,Amtabiria Kimataifa

Mchezaji wa kimataifa wa Tanzania anayecheza soka la Kulipwa nchini Morocco katika Klabu ya Diffaa El Jadid inayoshiriki ligi kuu ya Nchini Morocco ameguswa na Kiwango cha Kiungo wa Simba Said Hamis Ndemla.

Msuva ambaye kwasasa yupo nchini kwa mapumziko amesema kuwa uwezo wa Ndemla ni mkubwa sana na anaweza kucheza soka la kulipwa katika timu yeyote ile kubwa barani Afrika.

Msuva amesema alivutiwa sana na uwezo mkubwa aliouonyesha Ndemla katika mchezo kati ya Simba na Singida United Ndemla akitokea benchi kipindi cha Kwanza kuchukua nafasi ya Mwinyi Kazimoto na kusaidia kutengeneza magoli mawili kwa pasi mujarabu kutoka mguuni Mwake.

” Huwa nasema kila siku uwezo wa Ndemla kisoka ni Mkubwa ni vyema akaanza kuangalia nafasi ya kucheza soka nje ya Tanzania “

Hata hivyo kiungo huyo mwenye uwezo mkubwa sana wa kupiga kiufundi pasi za Mwisho na uwezo mkubwa wa Kupiga pasi ndefu na mashuti makali amewahi kufanya majaribio huko Sweden na uongozi wa Simba pamoja na wakala wake Jamal Kisongo kutangaza kuwa amefuzu majaribio lakini mpaka leo hakuna kinachoendelea juu ya safari yake kwenda Sweden.

Hata hivyo Ndemla kwa taarifa za ndani zinadai kuwa amebakiza miezi minne mkataba wake na Simba kumalizika kwahiyo huenda chochote kinaweza kutokea

Leave a comment