Home Michezo Msuva aondoka rasmi Yanga

Msuva aondoka rasmi Yanga

268
0

Baada ya tetesi za kuondoka Yanga kuzagaa, hatimaye mshambuliaji wa klabu ya Yanga Simon Msuva amethibitisha taarifa zake za kuondoka na kuelekea nchini Morroco kujiunga na klabu ya Difaa Al Jadida ambayo ni washindi wa pili wa ligi kuu Morroco.

Msuva amesema amefuata taratibu zote ambapo viongozi wote wa pande mbili wameafikiana na kufanya biashara, na anaamini ipo siku atarudi kuitumikia Yanga tena ila mpaka nitimize malengo yangu ya kucheza soka la kulipwa Ulaya.

“Kila kitu kipo tayari nasubiria viza tu itoke, nitaelekea Morocco kujiunga na klabu ya Difaa Al Jadida (washindi wa pili ligi kuu Morocco). . Naondoka Yanga SC , timu iliyonilea na kunipa mafanikio . . Siondoki kwa ubaya ndio maana nimefuata taratibu zote na viongozi wote wa pande mbili wameafikiana na kufanya biashara”. Amesema Msuva.

“Naamini ipo siku nitarudi kuitumikia Yanga tena ila mpaka nitimize malengo yangu ya kucheza soka la kulipwa Ulaya na kuwa miongoni mwa wanasoka waliofanikiwa nchini, baada ya Morocco Mungu akijalia basi itakuwa Ureno lakini hasa hasa ni Spain maana nina uwezo wa kucheza La Liga .

. Ahsante wana Yanga kwa ushirikiano mlionipa naamini kupitia kipaji changu kuna furaha nimewapa” alisema msuva alipozungumza na EATV.