Home News MUSIBA ADAI LISSU, CHADEMA WAANDAA WARAKA KUICHAFUA SERIKALI, RAIS

MUSIBA ADAI LISSU, CHADEMA WAANDAA WARAKA KUICHAFUA SERIKALI, RAIS

1873
0

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

MWANAHARAKATI huru anayejinasibu kuwa Mfuasi wa Rais John Magufuli, Cyprian Musiba amedai kuwa Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu kwa kushirikiana na Chadema wemeandaa mkakati wa kuichafua serikali na Rais.

Madai hayo amayetoa leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari na kusema kuwa kuna waraka maalumu ambao uliandaliwa na viongozi wa Chadema tangu Lissu alipokuwa akipatiwa matibabu nchini Kenya.

“Tundu Lissu anakaribia kurudi nchini, taarifa zinasema ni Januari 15, 2019, viongozi waliuandaa waraka akiwa Kenya  wakati akiendelea kutibiwa wakampa mkewe ili akipata nafuu  akabidhiwe, na akiwa huko Ubelgiji Mbowe alikwenda huko kuongeza data kwenye waraka huo,” alisema Musiba.

Aidha amedai kuwa waraka huo utaanza kusambazwa kwenye vyombo vya Magharibi, mitandao ya kijamii na atakapowasili nchini atazungumza na vyombo vya habari juu ya tukio la kushambuliwa kwake kwa risasi.

“Na akifika atazungumza na vyombo vya habari, atazungumzia kupigwa kwake risasi na tuhuma zake atazielekeza kwa serikali na kumdharirisha Rais, imetengenezwa kwa ajili ya kuichafua serikali, nchi na Rais, ni mwambie tu Lissu aache,” alibainisha Musiba.

Septemba 7, 2017 Mbunge huyo kwa tiketi ya Chadema alishambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana akiwa Bungeni Dodoma na kujeruhiwa vibaya ambapo hadi sasa yupo nchini Ubelgiji alipokwenda kwa ajili ya matibabu.

Wakati huo huo Musiba amedai kuwa Katibu Mkuu wa cha Wananchi CUF Maalim Seif alipokuwa Barani Ulaya mwishoni mwa mwaka uliopita Taasisi ya IRI ilimpa dola za Kimarekani bilioni 3 ili kuhakikisha anaivuruga Zanzibar.

“Watanzania wawe makini na mtu huyu, Maalim ni mtu hatari sana kwa nchi yetu, anataka kuivuruga nchi,” alisema.

Katika hatua nyingine Mwanaharakati huyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya CZI inayaozalisha magazeti ya Tanzanite na Fahri Yetu alitaja majina ya watu wadaodukua magazeti hayo kwa lengo la kumgombanisha.

Majina hayo ni Tumaini Makene (Chadema), Addo Shaibu, Mohamed Babu (ACT-Wazalendo), Monalisa Joseph Ndala, Abdallah Hamis (Mwandishi Jamvi la Habari) na Arani Kiluvia.

Alituhumu kuwa kudukuliwa kwa magazeti hayo ni mkakati wa Chama cha ACT-Wazalendo kwani kimeapa kupamana naye hivyo na yeye yupo tayari kwa mapambano.