Home Burudani MUSIBA ASONONESHWA WASANII KUJIREKODI PICHA ZA UTUPU PASIPO MAMLAKA KUWACHUKULIA HATUA

MUSIBA ASONONESHWA WASANII KUJIREKODI PICHA ZA UTUPU PASIPO MAMLAKA KUWACHUKULIA HATUA

1229
0
MWANAHARAKATI huru Cyprian Musiba ameeleza kusononeshwa na vitendo vya wasanii nchinikujirekodi picha za utupu na kisha kuziweka mitandaoni huku vyombo vyenye mamlaka vikishindwa kuwachukulia hatua zinazostahiki.

 

Mwanaharakati Huru, Cyprian Musiba akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam.
Musiba ameeleza hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu mambo mabalimbali yanayoenelea nchini leo jijini Dar es Salaam.
“Nimesononeshwa na ‘Trend’ ya wasanii kujirekodi picha za utupu huku wenye mamlaka wakikaa na kuleta siasa kwenye mambo ya msingi. Ningekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ningeifyekelea mbali BASATA,” alisema Musiba.
Aidha amehoji vitendo vya wasanii wakubwa kama Diamond Platinium, Wema Sepetu, Irene Uwoya kuweka picha hizo za jinsi hiyo bila kuchukuliwa hatua ambapo ameuliza kuwa wao ni kananani hadi wanaachwa na kuharibu watoto.
Akizungumza juu ya Amber Rutty Musiba amesema kuwa angetakiwa awe gerezani kwa video ile aliyojirekodi na kuweka mitandaoni.
Alishauri vyombo vyenye mamlaka kuwachukulia hatua wasanii hao kwa kuwafunga gerezani kwa matendo hayo yanayoharibu nchi na jamii kwa ujumla.
Katika hatua nyingine akizungumzia suala la korosho la mkoani Lindi amewataka wananchi mkoani humo kuwa makini na wanasiasa amabo wanalengo la kuwachonganisha na serikali kutokana na kwamba suala hilo serikali imeshaanza kulichukulia hatua.
“Nashauri Rais awafunge miaka 100 watu wote wanaotaka kuigawa nchi,” alisema.
Pia Mwanaharakati huyo ameeleza kuwepo kwa watu ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ambao wameanzisha harakati za kuelekea kusaka urais mwaka 2020, Serikalini na vyama vya upinzani ambao lengo lao ni kutaka kudhoofisha utendaji wa Rais na Serikali yake.
Alisema watu hao wanafahamika na kuwataka waache mikakati hiyo kwani hadi sasa anayetambulika kikatiba kuwa Rais wa nchi hii ni Dk. John Magufuli hivyo wamuache afanye kazi zake ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa miradi mbali mbali.
Kwa upande mwingine Musiba amemtuhumu Kiongozi wa Chama cha ACT- Wazalendo Zitto Kabwe kuwa ni fisadi kutokana ni kile alichodai kuwa kiongozi huyo amefanya matumizi mbalimbali ya zaidi ya sh.milioni 600 huku akihoji alipozipata.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Zitto Kabwe, alipoulizwa juu ya shutuma hizo, Katibu wa Itikadi, Mawasiliano na Uenezi wa ACT-Wazalendo Ado Shaibu, alijibu kwa niaba yake na alisema hawawezi kujibu kwa kile alichodai kwamba shutuma hizo zinaibuliwa zikiwa na lengo la kutaka kufunika masuala ya msingi kama ya usalama wa nchi na Koroshi yasijadiliwe kwa upana wake.