Home News MUSIBA ATII AGIZO LA SERIKALI, AHOJIWA NA IDARA YA HABARI (MELEZO)

MUSIBA ATII AGIZO LA SERIKALI, AHOJIWA NA IDARA YA HABARI (MELEZO)

1628
0
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MKURUGENZI Mtendaji wa Kampuni ya CZI amabye ndiye mmiliki wa Gazeti la Tanzanite Cyprian Musiba ametii agizo la serikali lililomtaka kufika Idara ya Habari (Maelezo) kuojiwa kutokana na gazeti lake kuandika habari iliyowataja vigogo 14 kwa madai kuwa ni hatari kwa nchi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya CZI Cyprian Musiba akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo pichani) jinini Dar es Salaam.
Hatua hiyo imekuja baada ya jana Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe kuagiza Idara ya Habari (Maelezo) kumhoji mmiliki na Bodi ya Uhariri ya Gazeti la Tanzanite,kwa kuandika habari (Vigogo 14 hatari kwa nchi yatajwa) yenye tuhuma za kisiasa dhidi ya viongozi mbali mbali.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam baada ya mahojiano, Musiba alisema ametii agizo hilo la serikali kwa sababu hayupo juu ya sheria.
“Niliitwa jana, nilipewa taarifa ya kuitwa, taarifa yenyewe ilikuwa imetolewa na Mh. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe baada ya moja ya vyombo vyangu kutoa taarifa kuhusiana na hayo amabyo mnayajua,” alisema Musiba.
“Sasa nchi hii inaendeshwa kwa sheria, na mimi kama Mtanzania siwezi na kamwe sitoweza kukaidi amri ya serikali kwa hiyo nimekuja hapa kwa kutii amri ya serikali Kwa sababu ambazo zilinitaka nifike, na tumefanya mazungumzo marefu tu na kwa kweli yalikuwa ni mazungumzo mazuri,” aliongeza.
Aidha Musiba aliahidi watanzania na wananchi wanaosoma vyombo vyake kuwa wataendela kufuata miiko na maadili ya vyombo vya habari na kuwahakikishia kuwa hatatumia vyombo vyake kupotosha.