Home Michezo Mzee Akilimali wa Yanga Afunguka Haya Mazito Baada ya Simba Kupewa Point...

Mzee Akilimali wa Yanga Afunguka Haya Mazito Baada ya Simba Kupewa Point Tatu za Mezani

83
0
Kamati ya Saa 72 ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) iliipa Simba pointi tatu baada ya kubainika Kagera Sugar ilimchezesha Mohammed Fakhi mwenye kadi tatu za njano katika mchezo wao ulioisha kwa Simba kufungwa mabao 2-1.
Sasa Katibu wa Baraza la Wazee wa Yanga, Mzee Ibrahim Akilimali ameibuka na kusema, TFF imefanya kitendo cha ajabu cha kukubali kuwapa Simba pointi za haramu na wao hawataweza kukubali. Kutokana na pointi ilizopewa, Simba sasa ipo kileleni katika msimamo wa Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 61 ikifuatiwa na Yanga yenye pointi 56. Hata hivyo, Yanga ina mchezo mmoja mkononi.
Mzee Akilimali alisema, wao hawatetei kwa kuwa wana ushindani wa kuwania ubingwa na Simba, isipokuwa wanachotaka haki itendeke kwa wote na siyo kwa baadhi tu.
“Kiukweli nikiwa kama Katibu wa Wazee wa Yanga hatukubaliani na kitendo cha TFF kuwapa hizo pointi za haramu Simba, siyo kwamba wote tunawania ubingwa, hapana, isipokuwa tunataka haki itendeke.
“Haiwezekani timu nzima washindwe kuwa na taarifa sahihi hivyo lazima tutaenda mbele, binafsi mimi ni msemaji wa wazee wenzangu ambao nipo pamoja na viongozi wangu wa juu wa kutaka kuona uchunguzi wa kina ili ukweli ujulikane.
“Lakini tutaandamana hadi kwa waziri halafu mahakamani wao si wamemwaga mboga, sisi tunamwaga ugali ili nchi ifungiwe kabisa na Fifa (Shirikisho la Soka la Kimataifa),” alisema Mzee Akilimali.

Leave a comment