Home Michezo Nahodha wa Bayern Philipp Lahm atangaza kustaafu mwisho wa msimu

Nahodha wa Bayern Philipp Lahm atangaza kustaafu mwisho wa msimu

20
0

MICHEZO. Nahodha wa Bayern Munich Philipp Lahm, aliyekuwa nahodha wa timu ya taifa ya Ujerumani walipotwaa Kombe la Dunia mwaka 2014, ametangaza kwamba atastaafu mwisho wa msimu.

Mchezaji huyo wa miaka 33 ametangaza uamuzi huo baada ya Bayern kushinda mechi ya hatua ya 16 bora katika michuano ya Kombe la Ujerumani dhidi ya Wolfsburg.
Ilikuwa mechi yake ya 501 kwake kuchezea viongozi hao wa Bundesliga.
“Ninaweza kuendelea na mtindo wangu wa uongozi, kujitolea kila siku, kila kipindi cha mazoezi, hadi mwisho wa msimu. Ninaweza kuendelea kufanya hayo msimu huu lakini si zaidi ya hapo,” amesema.
Hii ina maana kwamba ataondoka klabu hiyo mwaka mmoja kabla ya mkataba wake kumalizika.
Amesema amekuwa akitafakari kuhusu uamuzi huo kwa zaidi ya mwaka mmoja.
Alicheza mechi yake ya kwanza katika kikosi cha wachezaji wakubwa Bayern mwaka 2002 na ameshinda mataji saba ya Bundesliga akiwa na klabu hiyo, pamoja na Kombe la Ligi ya Klab
Alitangaza kustaafu kutoka kwa timu ya taifa baada ya kushinda Kombe la Dunia nchini Brazil mwaka 2014.