Home News NAIBU WAZIRI SIMA AZINDUA RIPOTI YA TAKWIMU ZA MAZINGIRA YA MWAKA 2017...

NAIBU WAZIRI SIMA AZINDUA RIPOTI YA TAKWIMU ZA MAZINGIRA YA MWAKA 2017 JIJINI DODOMA

1016
0

Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe. Mussa Sima akikata utepe kuzindua Ripoti ya Taifa ya Takwimu  za Mazingira ya mwaka 2017 leo Jijini Dodoma kwa niaba ya Waziri wan chi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba.

Mtakwimu mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS)  Bw. Pius Kasikana akiwasilisha mada wakati wa hafla ya kuzindua Ripoti ya Taifa ya Takwimu  za Mazingira ya mwaka 2017 leo Jijini Dodoma.

Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe. Mussa Sima akionesha Ripoti ya Taifa ya Takwimu  za Mazingira ya mwaka 2017 leo Jijini Dodoma mara baada yakuizindua leo Jijini Dodoma.

Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe. Mussa Sima akimkabidhi Ripoti ya Taifa ya Takwimu  za Mazingira ya mwaka 2017 Mkurugenzi wa Shughuli za Kitakwimu Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bw. Irenius Ruyobya leo Jijini Dodoma.

Meneja wa Takwimu za Bei na Ajira Bi Ruth Minja akiwasilisha mada wakati wa hafla ya kuzindua  Ripoti ya Taifa ya Takwimu za Mazingira ya mwaka 2017 leo Jijini Dodoma.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu Ardhi Dkt. Anes Mahenge akiwasilisha mada wakati wa uzinduzi wa Ripoti ya Taifa ya Takwimu  za Mazingira ya mwaka 2017 leo Jijini Dodoma.
(Picha zote na Frank Mvungi- MAELEZO
…………………….
Na.Alex Sonna,Dodoma
Naibu Waziri wa Wizara ya Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na mazingira Mussa Sima amesema kuwa ifikapo mwaka 2050 bahari zitakuwa zinatoa plasitiki zaidi kuliko samaki kutokana na taka hizo kuingia baharini mwaka hadi mwaka.
Naibu Waziri Sima amayasema hayo Jijini Dodoma  wakati akizundua ripoti ya Taifa ya Takwimu za Mazingira mwaka 2017 Tanzania bara huku akisema kuwa tani milioni nane za plastiki huingia baharini kwa mwaka.
Mhe.Sima amesema kuwa  kwa mujibu wa ripoti ya mazingira iliyoandaliwa na shirika la kimataifa ya mazingira ya mwaka 2017 ambayo pia imebaini kuwa ni asilimia 30 ya taka zote duniani kukusanywa na kudhibitiwa.
“Kutokana na Takwimu hiyo tunatakiwa kuhakikisha kuwa tunatunza mazingira yetu vizuri na kuhifadhi taka ili kuendelea kuzalisha samaki kwa wingi ili tusifike hatua hiyo ya kuwa na plastiki nyingi kuliko samaki,” amesema Sima.
Aidha amesema kuwa  serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wamefanya jitihada kubwa  katika kuboresha hali ya mazingira ikiwa kama nguzo moja wapo ya maendeleo endelevu kwa taifa letu
Kwa Upande wa  mtakwimu kutoka ofisi ya NBS Yohana Yakurwa akiwasilisha mada hiyo amesema kuwa uzalishaji, takwimu zinaonyesha kuwa  mwaka 2013 hadi 2017, kwa wasitani ni asilimia 20 peke ya maji taka yanayozalishwa katika jiji la Dar es salaam yanayokusanywa na kudhibitiwa ambapo takribani 80 ya maji hayo yanatupwa kwenye mazingira bila kutibiwa.
Akiongelea kuhusu uzalishaji na usimamizi wa taka ngumu Tanzania bara, alisema inakadiriwa uzalishaji wa kata hizo kwenye manispaa zote Tanzania bara zaidi ya tani 10,000  kwa siku ambapo takribani asilimia 80 hadi 90 ya taka zinazozalishwa nchini hazikusanywe.
Hata hivyo Bw.Yakurwa amesema kuwa taka za majimbani zinachangia kwa asilimia 60 ya taka ngumu zinazozalishwa kila siki na hutupwa kwa kuchimbiwa chini au kuchomwa na uzalishaji huo umekuwa ukiongezeka mwaka hadi mwaka.
Naye Meneja wa takwimu za mazingira ofisi ya Taifa ya takwimu Rose Minja  amesema kuwa ripoti hiyo ina mada zilizohusa maeneo makuu sita ambayo ni  hali na ubora wa mazingira, rasimilimali na mazingira na matumizi yake, mabaki, majanga na matukio makubwa, makazi ya watu, afya ya mazingira, ushiriki usimamizi na ulinzi wa mazingira.
Bi.Minja amesema  kuwa muongozo huu unaonyesha kwa kina uhusiana uliopo  kati ya mazingira na shughuli za maendeleo ya kijamii na kiuchumi, na ni kwa namna gani shughuli za kiuchumi na shughuli za kimaendeleo zinaathari mazingira na ni kwa namna gani ya kuhifadhi wa mazingira ili ili kuwa endelevu.
Amesisitiza kuwa madhumuni  ya ripoti hii ni kutoa taarifa kuhusu mazingira,kuonyesha mabadiliko muhimu ya mazingira katika vipindi mbalimbali na sababu zinazosababisha mabadiliko hayo, kutoa takwimu bora za mazingira ili kuongeza ufahamu wa masuala ya mazingira katika jamii na kusaidia katika utungaji na ufuataliaji wa sera za uhifadhi wa mazingira, kutoa taarifa kwa umma ili kuongeza uelewa kwa jamii kwenye masuala ya mazingira na mabadiliko tabia nchi.
Aidha amesema kuwa ripoti hii  imeandaliwa kwa ushirikiano wa wataalamu wa takwimu za mazingira kutoka wizara, idara na taasisi za serikali  ambapo pia walipata msaada wa kitaalamu kutoka ofisi ya kimataifa takwimu kitengo cha mazingira pamoja na msaada wa kitaalamu kutoka sekretarieti ya jumuiya ya Afrika mashariki,
Bi.Minja amesema kuwa ripoti hiyo ni ya nne lakini ni ya kwanza kuandaliwa na ofisi ya Taifa ya takwimu kwa kutumia muongozo unaokubalika kimataifa wa uandaaji wa takwimu za mazingira.