Home News NBC na TRA Yatoa Elimu Ya Kodi Kwa Wafanyabiashara Wa Moshi Na...

NBC na TRA Yatoa Elimu Ya Kodi Kwa Wafanyabiashara Wa Moshi Na Arusha

1627
0
????????????????????????????????????

Mkurugenzi wa Biashara wa Benki ya NBC, Elvis Ndunguru (kushoto), akizungumza katika semina iliyoandaliwa na benki hiyo kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) iliyolenga kujadili umuhimu wa suala la ulipaji kodi kwa wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla. Semina hiyo ilifanyika mjini Arusha juzi.

Ofisa Elimu Mkuu wa Mlipa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Rose Mahendeka (kushoto),  akitoa mada kuhusu kodi kwa wafanyabiashara wa mji wa Arusha katika semina iliyoandaliwa na Benki ya NBC kwa kushirikiana na mamlaka hiyo mjini humo juzi ililenga kujadili umuhimu wa suala la ulipaji kodi kwa wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla.

Meneja wa NBC Kanda ya Kaskazini, Salma Yatera (kushoto), akizungumza na wafanyabiashara na wateja wa benki hiyo waliohudhuria semina kuhusu masuala ya kodi iliyoandaliwa na NBC kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mjini Moshi, Kilimanjaro jana.

Ofisa Elimu Mkuu wa Mlipa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Rose Mahendeka (kushoto),  akitoa mada kuhusu kodi kwa wafanyabiashara wa mjini Moshi katika semina iliyoandaliwa na Benki ya NBC kwa kushirikiana na mamlaka hiyo mjini humo juzi ililenga kujadili umuhimu wa suala la ulipaji kodi kwa wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla.

 

Maofisa wa NBC na wa TRA wakipiga picha ya kumbukumbu na baadhi ya washiriki wa semina waliyoiandaa kwa wafanyabiashara na wateja wao  mjini Moshi, Mkoani Kilimanjaro jana.