Ngoma: Sichezi Mechi ya Simba

0
Mshambuliaji wa Yanga, Donald Ngoma amewathibitishia mashabiki wa klabu hiyo hatacheza mechi ya Jumamosi dhidi ya Simba kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Ngoma amewambia mashabiki mubashara kupitia mtandao wake wa Facebook alipokuwa akifafanua habari kwamba amegoma kucheza.
“Wengi wanauliza kuhusiana na hali yangu, ukweli ni kwamba mimi ni majeruhi na sitacheza mechi ya Jumamosi, siwezi kucheza kwavile bado nina majeraha.”
Kuna watu wanazusha kwamba nimegoma kucheza, hakuna kitu kama hicho hayo ni maneno tu, mimi ninaumwa ntachezaje? mnatakiwa kuelewa afya ya mchezaji ni kitu muhimu kwenye maisha ya mpira.
“Nitakuwa nje ya uwanja kama wiki sita, wala mashabiki wasiwe na wasiwasi kuna Chirwa(Obrey) na Tambwe (Amissi) ni wanajeshi watapambana. Timu itafanya vizuri.”
Facebook Comments
Share.

About Author