NI HURUMA KWA VIJANA SINGANO MESSI NA KESSY KUPOTEA KATIKA SOKA LA TANZANIA - The Choice

NI HURUMA KWA VIJANA SINGANO MESSI NA KESSY KUPOTEA KATIKA SOKA LA TANZANIA

0

MESSIIHAKIKA KATIKA MAAMUZI YEYOTE MTU ANAPOTAKA KUFANYA, LAZIMA KUFIKIRIA KWA KINA BILA KUKURUPUKA NA KUPATA USHAURI MBALIMBALI KWA WATU SAHIHI.VIJANA WENGI HUKURUPUKA KATIKA MAAMUZI YAO AMA KWA KUFUATA MKUMBO AU KWA USHAWISHI WA KITU FULANI.

KWA TANZANIA MBWANA SAMATTA HAKIKA NI MFANO WA KUIGWA KWANI NI MVUMILIVU NA YUKO MAKINI KATIKA KUFANYA MAAMUZI.ALIWEZA KULETEWA FIGISUFIGISU ALIPOKUWA TP MAZEMBE LAKINI ALIVUMILIA KWA KUHESHIMU MKATABA NA HATIMAYE ALIWEZA KUONDOKA KWA BARAKA ZOTE NA LEO HII ANAKULA BATA TU UBELIGIJI.

KWA WACHEZAJI WETU HASA VIJANA WA HAPA HAKIKA LAZIMA KUJIRIDHISHA NA MAMBO MENGI KABLA YA KUFANYA MAAMUZI YA MSTAKABALI WA MAISHA YAO YA BAADAYE.MCHEZAJI YEYOTE LAZIMA UWE NA USIMAMIZI ULIO BORA NA WENYE UELEWA WA HALI YA JUU,KWA BAHATI MBAYA WENGI WAMEKUWA NA USIMAMIZI MBOVU NA MAAMUZI MABOVU.

KWA UPANDE WA SINGANO

HAKIKA TOKEA AONDOKE SIMBA NI KAMA AMEPOTEA KATIKA RAMANI YA SOKA TANZANIA KUTOKANA NA KUTO PATA NAMBA KATIKA KIKOSI CHA AZAM NA HIVYO KUHATARISHA KIWANGO CHAKE CHA SOKA KUPOROMOKA.HAKIKA WAKATI YUKO SIMBA ALIPATA NAFASI YA KUTOSHA KUWEZA KUCHEZA NA KUONEKANA ,NASEMA YAWEZEKANA KATIKA KIPINDI CHA MGOGORO KATI YA SIMBA NA SINGANO  ILIKUWA NDO KIPINDI KIZURI KWA MENEJA WAKE KUTUMIA UWEZO WAKE KUMALIZA MGOGORO KWA AMANI KULIKO NAYE KUCHOCHEA HADI ANAONDOKA NA KUHAMIA AZAM BILA KUWA NA BARAKA TOKA SIMBA.

KESSY

SWALA LA KESSY LIMEKUWA GUMZO SANA HAPA NCHINI NI KUTOKANA NA KILEKILE KUTO KUWA NA USIMAMIZI MZURI WA MAMENEJA.HAKIKA KESSY NAYE NI MMOJA WA WACHEZAJI AMBAYE KWA SASA NI KAMA AMEPOTEA KATIKA SOKA LA TANZANIA UKILINGANISHA NA ALIVYO KUWA SIMBA ALIWEZA KUPATA NAFASI YA KUCHEZA MARA KWA MARA .KWA YANGA INAKUWA VIGUMU KUTOKANA NA NAMBA ANAYOCHEZA KUZIBWA VIZURI NA JUMA ABDUL HIVYO KESSY MDA MWINGI HUKAA BENCHI

Facebook Comments
Share.

About Author