Home Michezo NI NGUMU KUAMINI ILA TAZAMA UJIONEE MWENYEWE WALICHOKISEMA YANGA JUU YA DIDA...

NI NGUMU KUAMINI ILA TAZAMA UJIONEE MWENYEWE WALICHOKISEMA YANGA JUU YA DIDA HAPA

133
0

UONGOZI wa Klabu ya Yanga umesema kuwa bado nafasi ya aliyekuwa mlinda mlango wa timu hiyo, Deogratius Munishi ‘Dida’, ipo japokuwa ameondoka klabuni hapo.

Dida amekataa kuongeza mkataba mwingine wa kuitumikia Yanga kufuatia mchakato wake wa kwenda kucheza soka la kulipwa Afrika Kusini.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa Yanga, Hussein Nyika, ameeleza kuwa, licha ya kuondoka kwa Dida katika timu hiyo, bado atakuwa na nafasi yake iwapo atahitaji kurejea kikosini hapo.

“Dida siyo mchezaji wetu kwa sasa kwani mkataba wake umeisha mwezi huu wa saba na sasa anakwenda Afrika Kusini kufanya majaribio, tulitaka kumuongeza mkataba mwingine lakini amekataa.

“Nafasi bao ipo wazi kwake aende kufanya majaribio na iwapo atarejea basi nafasi yake ipo, ila hatujui anakwenda timu gani,” alisema Nyika.