Nuh Mziwanda Akesha Akiomba Mapacha - The Choice

Nuh Mziwanda Akesha Akiomba Mapacha

0
MSANII wa muziki Bongo, Naftal Mlawa ‘Nuh Mziwanda’ amefunguka kuwa anakesha kila siku akimuomba Mungu amjaalie mke wake Nawal ambaye sasa ana mimba ya takriban miezi minne ajifungue watoto mapacha.
Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni, Nuh alisema kuitwa baba wawili imekuwa ni ndoto yake ya muda mrefu na anaomba itimie kwa mkewe huyo kipenzi. “Niseme tu wazi kwamba natamani sana mke wangu ajifungue mapacha.
Naamini furaha yangu itakuwa zaidi ikiwa hivyo lakini hata akiwa mmoja pia nitashukuru. Kikubwa naomba mke wangu ajifungue salama ili na sisi tuingie kwenye ulimwengu wa wazazi,” alisema Nuh.
Nuh alifunga ndoa na Nawal mwishoni mwa mwaka jana na ilielezwa kuwa, wakati mwanadada huyo akiolewa alikuwa tayari ameshanasa mimba.
Facebook Comments
Share.

About Author