OFFICIAL: Lwandamina akabidhiwa Yanga

0
 

img_5618

Geroge Lwandamina ametambulishwa rasmi kuwa kocha mpya wa Yanga SC akirithi nafasi ya kocha wa zamani wa klabu hiyo Hans van der Pluijm ambaye amepewa majukumu mapya ya kuwa Mkurugenzi wa Ufundi ndani ya klabu hiyo inayotetea ubingwa wake wa VPL ilioutwaa msimu uliopita.

Lwandamina amesaini mkataba wa miaka miwili utakaomuweka Jangwani.

img_5641

Makamu Mwenyekiti wa Yanga Clement Sanga amewatambulisha wawili hao ndani ya makao makuu ya klabu ya Yanga na kumkabidhi Lwandamina jezi ya Yanga ikiwa ni ishara ya utambulisho na kumkaribisha ndani ya klabu.

Pluijm pia ametangazwa rasmi kuchukua majukumu mapya ya kuwa Mkurugenzi wa Ufundi akiachana na masuala ya ukocha ndani ya klabu hiyo aliyoipa mafanikio makubwa ikiwa chini yake kama kocha mkuu.

img_5504

Lwandamina amekabidhiwa klabu ikiwa nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu Tanzania bara pointi mbili nyuma ya vinara wa ligi Simba ambao wanapointi 35 baada ya mzunguko wa kwanza kumalizika.

Kocha huyo (Lwandamina) aliifikisha Zesco United hatua ya nusu fainali kwenye michuano ya klabu bingwa Afrika msimu uliomalizika hivi karibuni, atakuwa na kibarua kuhakikisha anatetea taji la VPL, Azam Sports Federationa Cup (FA Cup) pamoja na kuhakikisha Yanga inafanya vizuri kwenye michuano ya kimataifa ambapo msimu uliopita ilifika hatua ya makundi ya kombe la shirikisho Afrika chini ya Pluijm

Facebook Comments
Share.

About Author