Okwi Gumzo wababe wengine Afrika watuma Ofa kumng’oa Simba
KIWANGO cha hali ya juu alichokionyesha mshambuliaji wa Simba na Raia wa Uganda Emmanuel Okwi kimefanya vigogo zaidi wa soka la Afrika kumtupia jicho.
Awali ilielezwa vilabu kutoka Afrika Kusini ikiwemo Kaizer Chief kumtupia jicho Straika huyo aliyewalaza na viatu Js Saoura ya Algeria kwa kuwafunga na kutoa Assist lakini pia hata manyanyaso akiwa uwanjani.
Inaelezwa kuwa kuna klabu kubwa kutoka nchini Misri imetuma ofa ya kutaka kumng’oa Okwi Simba baada ya kuelezwa kumfatilia kwa muda mrefu lakini zaidi kufurahishwa na uwezo wake aliouonyesha wakicheza na Js Saoura majuzi.