Home Uncategorized ONESHO LA TAMTHILIA YA MALKIA BIBI TITI MOHAMED LAFANA SANA

ONESHO LA TAMTHILIA YA MALKIA BIBI TITI MOHAMED LAFANA SANA

1728
0

Na Mwandishi Wetu, Pwani
KIKUNDI cha Sanaa cha Kaleleo usiku wa juzi Oktoba 26, 2018 kilifanya onesho la Tamthilia ya Malkia Bibi Titi Mohamed lililokuwa likionyesha jinsi mwanamke huyo shujaa alivyoshiriki kwa ujasili mkubwa kwenye harakati za kutafuta uhuru wa Tanganyika.
Kikundi cha Sanaa cha Kaleleo kikifanya onesho la Tamthilia ya Malikia Bibi Titi Mohamed kwenye Taasisis ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) katika TAMASHA la 37 la Kimataifa la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo.
Onesho hilo lilifanyika mkoani Pwani, Wilayani Bagamoyo kwenye Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) katika TAMASHA la 37 la kimataifa la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo lilifana sana na kwani lilikuwa kivutio kwa watazamaji.
Akizungumza baada ya onesho hilo Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya Africa Proper Education Network (APE Network) ambao ndiyo wathamini watamhtilia hiyo, Hermes Damian alisema tamthilia hiyo itaendelea kuoneshwa katika majiji mbali mbali nchini ambapo itaanzia katika jiji la Dar es Salaam kisha majiji mengine ambayo ni Arusha, Mwanza, Dodoma na Mbeya.
“Baada ya tamthilia hii ya Malkia Bibi Titi Mohamed kuoneshwa hapa, hivi karibuni tutaenda kulionesha jijini Dar es Salaam na Majiji mengine nchini, lengo ni kuifikia jamii na kuielimisha kupitia maigizo ya jukwaani,” alisema Damian.
Aliongeza kuwa baada ya tamthilia hii kukamilika wanamipango ya kuendelea kufanya tamthilia nyingine ambapo mipango yao ni kwamba kwa mwaka mmoja wawe wanafanya angalau tamthilia tano.
Alisema miongoni mwa tamthilia zilizopo katika mipango yao ni Nyerere na Safari ya Kanani, Tomboya na Morani.
Akizungumzia juu ya APE kujihusisha na michezo hii ya jukwaani alisema lengo ni kusaidia katika kuhifadhi utamaduni wetu na kueneza lugha ya kiswahili duniani pamoja na kuunganisha wasanii, taasisi za kiswahili na wananchi ili kushirikiana kukuza sanaa za maonesho hususani michezo ya kuigiza na kwatu kuweza kuwafikia watu wengi na hadhira zaidi siku hadi siku.
Aidha alikaribisha udhamini ama ufadhili wa makampuni na taasisis mbalimbali kwa namna mbalimbali, ambapo alitoa mfano kuwa wanaweza kuruhusu wadhamini na wafadhli kuweka matangazo yao ya biashara jukwaani ama ndani ya kumbi ya maonesho.
Kwa upande Mtunzi wa Tamthilia hiyo ambaye Pia ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu Huria cha anzania (OUT) Profesa Emmanuel Mbogo alisema lengo la tamthilia hiyo ni kutaka kuifunza jamii historia na watu waliohusika katika kumfukuza mkoloni kipindi cha kupigania uhuru wa Tanganyika.
Aliongeza kuwa lengo lingine ni kutaka kuonesha jinsi Bibi Titi Mohamed kama mwanamke alivyoshirika katika kupigania uhuru ambapo kwa kielelezo hicho kinaonesha kuwa mwanamke anaweza kufanya jambo katika jamii na kwa mafanikio tofauti na jinsi jamii inavyomchukulia mwanamke kuwa ni kiumbe dhaifu.
Naye Neema Mirambo mshirika katika tamthilia hiyo kama Malkia Bibi Titi Mohamed aliwataka wanawake kuamini kuwa wanaweza kuisaidia jamii kama alivyofanya Bibi Titi licha ya jamii yetu kumtenga mwanamke.
Habari katika picha kwenye Onesho hilo