Home News PATORANKING KUKIWASHA DAR LEO

PATORANKING KUKIWASHA DAR LEO

1792
0
Na Mwandishi Wetu,  Dar es Salaam
Mkali wa muziki kutoka Nigeria Patrick Nnaemeka Okorie, maarufu kama Patoranking ametua bongo kwa ajili ya kufanya tamasha kubwa linalotarajiwa kufanyika leo jijini Dar es salaam.

Akizungumza na wanahabari mkali huyo wa Nigeria amesema kuwa amefurahishwa kurudi Tanzania kwa mara nyingine kufanya tamasha kubwa ambalo ameahidi kufanya tamasha ambalo halijawahi kufanyika bongo na msanii wa nje.

Naye mkali wa bongo fleva CHEGGE CHIGUNDA amewashukuru waandaaji wa Tamasha hilo kwa kumchagua yeye kuwa mmoja ya wasanii watakaotumbuiza kwenye tamasha hilo kubwa la muziki.

Tamasha hilo lililoandaliwa na Buckets na Hugo

domingo LTD litakalofanyika katika ukumbi wa Buckets,Masaki pia litatumbuizwa na mkali kutoka kiwanda cha bongo fleva QUICK ROCKER(switcherBaba)CHEGGE CHIGUNDA na Grace kuanzia saa mbili usiku.