PICHA: Hili ndilo jina la mpira utakaotumika kwenye michuano ya EURO-2016. - The Choice

PICHA: Hili ndilo jina la mpira utakaotumika kwenye michuano ya EURO-2016.

0

Michuano ya Euro 2016 inatarajiwa kuanza rasmi leo nchini Ufaransa ambapo kutakuwa na mchezo mmoja utakaowakutanisha wenyeji Ufaransa dhidi ya  Romania katika mchezo utakaopigwa kunako dimba la Stade de France majira ya saa nne usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

BEAU-JEU-ADIDAS-001

Kama ilivyo ada katika michuano ya Ulaya, Amerika na hata ile ya  dunia kwa ujumla,huwa kunakuwa na mpira maalum unaoandaliwa kwa ajili ya michunao husika ambapo katika michuano ya Euro mwaka huu, mpira utakaotumika unajulikana kwa jina la Adidas Beau Jeu,”Beau Jeu” ni jina la kifaransa likimaanisha  ‘Beautiful Game’ au ‘Beautiful Play’ ambapo kwa Kiswahili maana yake ni Mchezo mzuri.

Mpira huu ulizinduliwa na Kampuni ya Adidas na kutambulishwa na mchezaji wa zamani wa Ufaransa Zinedine Zidane mwezi Novemba mwaka jana.

Facebook Comments
Share.

About Author