PICHA YA MKUDE, MSUVA WAKIWA PAMOJA NDANI YA GARI YAZUA GUMZO MTANDAONI - The Choice

PICHA YA MKUDE, MSUVA WAKIWA PAMOJA NDANI YA GARI YAZUA GUMZO MTANDAONI

0

 

Kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii, gumzo ni wachezaji wawili, Simon Msuva wa Yanga na Jonas Mkude wa Simba.
Wawili hao wanaonekana wakiwa katika gari moja, wengi mtandaoni wanaichukulia kama sehemu kuwa huenda Mkude ndiyo njiani kujiunga na Yanga kwa kuwa suala lake la usajili na Simba linaonekana kuwa na shida.
Kiuhalisia, Mkude na Msuva ni marafiki wa karibu kwa kuwa wote wako katika umri mmoja ‘aga mate’ na wamecheza pamoja sehemu mbalimbali kwa maana ya upinzani lakini wakiwa pamoja mfano timu za vijana na taifa.
Ingawa watu hawajaeleza au kujua kwamba picha hiyo ni ya hivi karibuni au ya kitambo.
Wanaojadili mitandaoni, wengi wanaamini Msuva anaweza kumshawishi kutua Yanga. Wako wanaomkaribisha na wengine wakionyesha hawana shida naye Yanga.

 

Kwa mashabiki wengi wa Simba, wengi wanapuuza kwa kusema “aende zake”, wako wanaonya kwamba awaangalie akina Ramadhani Singano na wengine na wengine wanamshauri kuwa makini wakiamini Yanga huua vipaji vya wachezaji wengi wanaotokea Simba. MJADALA UNAENDELEA
Share.

About Author