POLEPOLE Afunguka ya Moyoni Kuhusu Samatta..Afichua Kuwa Yeye ni Yanga Damudamu..!!! - The Choice

POLEPOLE Afunguka ya Moyoni Kuhusu Samatta..Afichua Kuwa Yeye ni Yanga Damudamu..!!!

0
Katibu wa itikadi, siasa na uenezi wa chama cha mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole amemtaja mshambuliaji wa RCK Genk, Mbwana Samatta kama mwanasoka pekee anayemvutia hapa nchini.
Akizungumza katika mahojiano maalum katika ofisi za gazeti la Mwananchi, Tabata Relini,  Polepole alisema juhudi za Samatta ambaye ni nahodha wa timu ya taifa,  Taifa Stars ndizo zinazofanya avutiwe naye.
“Napenda kuona vijana wetu wanapata mafanikio kwenye soka hivyo mchezaji wa soka ambaye ninampenda ni Mbwana Samatta.
Huyo tu kwa upande wangu ndiye anatosha kwa ndani na nje ya nchi na hakuna mwingine anayenivutia zaidi yake,” alisema Polepole.
Polepole alifichua kuwa yeye ni shabiki wa kutupwa wa klabu ya Yanga.
Credit – mwananchi
Facebook Comments
Share.

About Author