Home News PROFESA MKUMBO AZITAKA MAMLAKA ZA MAJI ZIWEKEZE KWENYE MIRADI

PROFESA MKUMBO AZITAKA MAMLAKA ZA MAJI ZIWEKEZE KWENYE MIRADI

1367
0
DSC_0070

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Profesa Kitila Mkumbo akizungumza na wadau mbalimbali wa maendeleo wakati wa semina ya miradi ya maji iliyofadhiliwa na Water Aid uliojengwa Kibondemaji na Toangoma.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Profesa Kitila Mkumbo amesema kuwa serikali imezitaka mamlaka za maji kujiendesha kikamilifu ikiwemo  kuwekeza moja kwa moja kwenye miradi ya maji.
 
Hayo ameyasema Profesa Mkumbo wakati wa semina iliyowahusisha wadau mbalimbali wa maendeleo inayohusu miradi ya maji ya Toangoma na Kibondemaji.
 
Amesema kuwa, kumekuwa na utelekezaji mbalimbali wa miradi ya maji unaofanywa na serikali kwa kuwekeza kikamilifu ila kwa sasa Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa kuwa kwa sasa mamlaka zote zianze kujiendesha.
 
Ameeleza kuwa, wadau mbalimbali wa maendeleo wamekuwa wanashiriki kwa kiasi kikubwa kwenye uwekezaji wa miradi ya maji na suala hilo limekuwa na mchango mkubwa sana kwa serikali.

Profesa Mkumbo amesema zaidi ya mamlaka za maji 14 nchini kote kwa sasa zinajiendesha zenyewe na wamefanikiwa kwa asilimia 100, ambapo mamlaka hizo ni Kama Dar es Salaam, Kilimanjarao, Arusha, Sumbawanga, Mtwara na zingine.

Akizungumzia mradi wa Toangoma na Kibondemaji, Mkumbo amesema kuwa utasaidia wananchi wa maeneo hayo kuachana na uharibifu wa mazingira kwa kutiririsha maji taka.

Kwa upande wa Mhandisi wa Maji wa Manispaa ya Temeke Damas Primy amesema Manispaa nzima ina kata 23 na idadi ya watu Milioni 1.3  na mradi Toangoma wa Kuchakata maji taka utawanufaisha zaidi wananchi kutokana na faida zitakazopatikana kwenye maji hayo.

Primy amesema kuwa, manispaa imeshirikiana na nMamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) katika ujenzi wa mradi huo wa kuchakata maji taka uliodhaminiwa na Water Aid.

Mradi huo utawasaidia wananchi walio na kipato kidogo kuweka kuondoa maji hayo majumbani kwao kutokana na gharama za usafirshaji wa maji taka hayo, na utasaidia katika kuondoa uchafu majumbani, kupunguza magonjwa ya mlipuko, kuongeza kipato kutokana na mazao yanayotokana na maji hayo ikiwemo mbolea, maji kutumika kwa shughuli za kilimo, upatikanaji wa Biogas.

Kwa upande wa DAWASA, wameweka wazi kuwa mradi huu ulianza 2016 na kumalizika Mei 2018 na utakuwa ni wa majitaka na wakiwa umefadhiliwa a Water Aid ila wao kama mamlaka ya maji ya Mkoa wa Dar es Salaam wameweza kuwa nao kwenye masuala ya miundo mbinu na mfumo huo wa uchakataji maji ni wa asili na hautatumia dawa.

DSC_0112
Mkurugenzi wa Tanzania wa Water Aid Ibrahim Kabole akielezea jambo kwa  Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Profesa Kitila Mkumbo kuhusina na mradi wa uchakataji maji uliofadhiliwa na tasisis yao uliojengwa Kibondemaji na Toangoma.
DSC_0090
Mwakilishi kutoka Chuo cha Ardhi Edward Ruhinda akizungumzia mradi wa Uchakataji maji na namna wananchi wanavyo haribu mazingira kutokana na maji taka.

DSC_0074
DSC_0080

Wadau mbalimbali wa maendeleo wakiendelea kufuatilia  semina ya mradi wa uchakataji maji taka uliojengwa Kibonde maji na Toangoma.