Home Burudani Q-CHIEF ATANGAZA KUACHA MUZIKI

Q-CHIEF ATANGAZA KUACHA MUZIKI

63
0

“Nilipata umaarufu nikiwa na umri mdogo wa miaka 19, nilizungukwa na watu ambao ni wema na wabaya. Presha ya kupambana na umaarufu, ilikuwa kubwa. Imenisumbua na mpaka nikajiingiza kwenye matendo yaliyoniondoa kwenye njia sahihi.” “Maisha ninayoishi naona yanadhalilisha Bongo Fleva, naona bora niachane na hili, niangalie shughuli nyingine.” “Mimi naacha muziki lakini sio niwe kama kama wenzangu Mzee Yusuph na Suma Lee, naacha kutokana na sababu zangu. Nautua huu mzigo mzito ambao nimeshindwa kuendelea kuubeba.” Nilishafikiria kufanya mambo mengi ya ajabu kuliko hata hili la kutangaza kuacha muziki. Ningeweza kufanya vibaya ambavyo visingempendeza Allah na familia yangu “Kinachoniuma naacha muziki nikiwa naona bado naona nafasi yangu kwenye muziki, nasikiliza nyimbo zinazopigwa bado naona ningeweza kupita katikati yao na kutengeneza barabara yangu.” @qchillasavimbi @qchief1 #chillaonxxl