RAIS Magufuli Afanya Uteuzi Mpya…

0


UKULU, DAR: Taarifa kutoka kwa Katibu Mkuu Balozi Kijazi zinasema Rais Magufuli amemteua aliyekuwa Kamishna Msaidizi wa Uchimbaji Mdogo, Mhandisi Benjamin Mchwampaka kuwa Kamishna Mkuu wa Madini.

Kabla ya hapo alikuwa Kamishna Msaidizi wa sehemu ya uchimbaji mdogo wa madini. Aidha uteuzi wake umeanza tarehe 19 April, 2017.

Wakati huo huo Rais amemteua Adelarnus Kilangi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli(Petrolium Upstream Regulatory Authority – PURA). .

Aidha Bi. Kilangi alikuwa Mkurugenzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino Tanzania(SAUT) Kampasi ya Arusha. Pia uteuzi wake umeanza tarehe 19 April, 2017.

Facebook Comments
Share.

About Author