RAIS wa CAF Akataa Kupokea Mshahara...!!! - The Choice

RAIS wa CAF Akataa Kupokea Mshahara…!!!

0
Rais mpya wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Ahmad Ahmad amekataa kupokea mshahara wake kutoka kwa shirikisho hilo.
Akitoa sababu za kukataa kupokea mshahara huo, Ahmad alisema kuwa shirikisho hilo haliheshimu uongozi au utawala bora na haki za wafanyakazi.
“Nimekataa mshahara wa CAF kwa sababu rahisi, haiheshimu utawala bora. Mishahara ya waajiriwa wote wa CAF, kuanzia ngazi ya uongozi hadi kwenye Kamati na rais mwenyewe, kote inapaswa kuwe na uwazi,” Ahmad ameiambia BBC.
Ahmad ambaye ni raia wa Madagascar ameweka wazi msimamo wake kuhusu mshahara, wakati ambapo anafanya mkutano wake wa kwanza leo na viongozi waandamizi wa CAF kabla ya kushiriki mkutano wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), utakaofanyika Alhamisi ya juma hili.
Ajenda kubwa ya mkutano wa leo ni namna ya kufanya mageuzi ya kiutawala katika shirikisho hilo.
Ahmad aliingia madarakani mwezi Machi kupitia uchaguzi, baada ya kumwaga Issa Hayatou’s aliyeongoza kwa takribani miongo mitatu.
Facebook Comments
Share.

About Author