RASMI: YANGA WAMSAJILI KIUNGO HUYU KUTOKA ZANZIBAR HEROES

0
Yanga yazishinda Simba na Azam FC, katika mbio za kumwania kiungo wa JKU ya Feisali Abdallah kwa mkataba wa miaka mitatu

Hatimaye klabu ya Yanga imefanikiwa kushinda mbio za kuwania saini ya kiungo wa timu ya taifa ya Zanzibar Heroes na klabu ya JKU Feisali Abdallah ‘Totoo’

Msemaji wa Yanga Godlisten Chicharito ameiambia Goal, kuwa wamempa mkataba wa miaka mitatu na mchezaji huyo anatarajiwa kuanza kuichezea timu hiyo msimu ujao wakati ambao usajili wake utapitishwa na Shirikisho la soka TFF.

“Nikweli tumemsajili Feisali kwa mkataba wa miaka mitatu na mashabiki wa Yanga wataanza kumuona uwanjani akiwa na kikosi cha Yanga msimu ujao,” amesema Chicharito.

Kiungo huyo aliyetamba akiwa na Zanzibar Heroes kwenye michuano ya Chalenji nchini Kenya pamoja na michuano ya Kombe la Mapinduzi ambayo inakamilika leo hapa Zanzibar alikuwa pia anawaniwa na klabu za Azam FC na Simba.

1,954 total views, 3 views today

Facebook Comments
Share.

About Author