Home Michezo REAL MADRID WATWAA UBINGWA WA LA LIGA, SHANGWE ZATAWALA JIJI LA MADRID

REAL MADRID WATWAA UBINGWA WA LA LIGA, SHANGWE ZATAWALA JIJI LA MADRID

137
0

Real Madrid imefanikiwa kutwaa ubingwa wa LaLiga kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2012 baada ya kuifunga Malaga mabao 2-0, jana usiku.

Ubingwa huo wa Ligi Kuu ya Hispania msimu wa 2016/17 ulipatikana kutokana na mabao ya Cristiano Ronaldo na Karim Benzema.

Kutokana na ushindi huo Madrid imefikisha pointi 90 ikifuatiwa na Barcelona yenye pointi 87.

Akizungumzia juu ya ubingwa huo, Zinedine Zidane alisema ulikuwa ni ushindi muhimu, amewapongeza wachezaji wakem haku akidai kuwa sasa akili zao wanazipeleka kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ambapo watacheza dhidi ya Juventus, wiki ijayo.

“Ronaldo yupo siku zote unapomhitaji, alikuwa katika ubora wake na katika muda unaotakiwa, lakini ushindi huu ni maalum kwa ajili ya wachezaji wote,” alisema Zidane.