Home Michezo Rekodi 3 alizoweka Papy Tshishimbi Iringa

Rekodi 3 alizoweka Papy Tshishimbi Iringa

256
0

Yanga jana walifanikiwa kupata Ushindi kwa Mara ya Kwanza kwenye uwanja wa Samora wakicheza Na Lipuli, Yanga haikuwahi kupata Ushindi katika uwanja wa Samora wakicheza na Lipuli na Jana ilikuwa ni Mara ya Kwanza kwa Yanga kuvunja Mwiko Huo.

Lakini Katika Mchezo huo kiungo kutoka Congo Papy Kabamba Tshishimbi ameweka Rekodi 3 Katika Mchezo Huo.

Rekodi ya Kwanza

Papy Tshishimbi amekuwa mchezaji wa Kimataifa wa Kwanza Kwa Yanga kufunga Goli katika uwanja wa Samora, Kabla hakuna ambaye aliwahi kufanya hivyo kwa Yanga.

Rekodi ya Pili.

Ameweka rekodi ya Kupiga pasi nyingi zaidi kwa klabu yake ya Yanga kwenye Mchezo wa Jana kwani amepiga jumla ya Pasi 44 katika mchezo Huo.

Rekodi ya tatu

Imekuwa ni Goli lake la kwanza kwenye Ligi kwani toka Ligi hiyo Ianze msimu Huu Tshishimbi hakuwahi Kufunga Goli na Jana ameweka Rekodi Huko Iringa kwa Kufunga goli lake la Kwanza.

Yanga katika mchezo huo msomaji wa Kwataunit Ilifanikiwa kupata Ushindi wa jumla ya Bao 2 kwa 0 Magoli ya Yanga yakifungwa na Papy Kabamba Tshishimbi , Na Goli la Pili likifungwa na Pius Charles Buswita ambaye alimpa Pasi Obrey Chirwa, Chirwa akakimbia na Mpira na Kupiga Krosi kwa Buswita tena Ambaye alimpiga Chenga Kipa na Kufunga Goli.

Leave a comment