Rigobert Song afikishwa hospitali kwa matatizo ya ubongo - The Choice

Rigobert Song afikishwa hospitali kwa matatizo ya ubongo

0

 

 

 

 

 

Nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya Cameroon na kocha wa sasa wa timu ya taifa ya vijana wadogo ya Cameroon, Rigobert Song amefikishwa mjini Yaounde, Cameroon baada ya kuugua ghafla.

Taarifa kutoka vyanzo vya habari vya Cameroon, zinaeleza kuwa Song amepatwa na tatizo katika mishipa yake ya kwenye ubongo (cerebral vascular) wakati akiwa nyumbani kwake Odza.

Baada ya kuugua ghafla, Song alifikishwa katika Hospitali ya Messa ambapo yupo mpaka sasa akiwa katika uangalizi maalumu wa madaktari ili kuhakikisha anarejea katika hali yake ya awali.

MO Blog itaendelea kukuletea taarifa kuhusu hali ya mkongwe huyo wa soka barani Afrika.

Share.

About Author