Ronaldinho apata kazi mpya ndani ya Barcelona. - The Choice

Ronaldinho apata kazi mpya ndani ya Barcelona.

0

Dinho Gaucho bila shaka ni mchezaji ambae yupo kwenye historia ya club hiyo kutokana na alichokifana ndani ya miaka 5. Dinho alikua kipenzi cha mashabiki wengi duniani na kuiongezea clbu hiyo mashabiki wengi ambao wengi wapo hadi leo.

Sasa hivi Dinho amepata kazi nyingine official chini ya club yake hiyo ya zamani. Tangu aihame hakuna na mkataba mwingine wa kuiwakilisha club hiyo, lakini sasa hivi atakua balozi wa dunia nzima wa club ya Barcelona.

Dinho atakua na majukumu ya kuiwakilisha club hiyo kwenye vitu na matukio mbalimbali yanayohusu club hiyo. Kutokana na ushawishi mkubwa ambao Dinho anao, inategemewa kuwa kivutio kikubwa kwa watu mbalimbali.

Dinho akizungumzia kazi yake hiyo mpya alisema,“Nina furaha sana, watu wachache sana wanapata nafasi ya kuwa balozi wa Barcelona. Nime miss kila kitu cha hapa kwasababu nilitumia muda mwingi sana kuwa hapa. Niliacha marafiki wengi sana na sikurudi Nou Camp hadi sasa hivi. Kurudi hapa na kuwa na kazi kama mchezaji ni kitu kizuri sana kwangu, Watu walikua wahawahusishi jina langu moja kwa moja na Barcelona lakini siku zote nilijiskia kama balozi”.

Moja ya kazi za Dinho zitakua ni kushiriki kwenye matukio mbalimbali ya Barcelona ya kijamii na kibiashara dunia nzima,

Share.

About Author