Home Michezo Sababu ya Mavugo kuachwa kikosi kilichoenda Djibouti hii Hapa,Simba wafunguka

Sababu ya Mavugo kuachwa kikosi kilichoenda Djibouti hii Hapa,Simba wafunguka

183
0

Manara wametoa ufafanuzi kuhusu kuachwa kwa Mabugo baada ya ya Kikosi cha Majina ya Wachezaji 20 wa Simba waliosafiri kwenda Djibouti kwaajili ya Mchezo wa Kombe la Shirikisho barani Afrika Mkondo wa Pili kati ya Gendarmerie dhidi ya Simba.

Katika Kikosi kilichoenda Djibouti Jina la Mavugo halipo na baadhi ya watu wameshaanza kutengeneza sababu zao huku wengi wakiamini kuwa ni uwezo mdogo wa Uwanjani ambao amekuwa akiuonyesha uwanjani hasa katika mchezo kati ya Mwadui na Simba ambao licha ya Kuingia Sub alikuja kufanyiwa tena Sub.

Mkuu wa Kitengo cha habari na mawasiliano klabu ya Simba Haji Sunday Manara ameithibitishia  kuwa Mavugo hajajumuishwa kwenye safari hiyo kutokana na kuwa kwenye matatizo kwenye Usajili wake kwenye michuano Hiyo.