Sababu za Aubameyang kutoka cheza dhidi ya Sporting Lisbon

0

Mshambuliaji Pierre Emerick Aubameyang ambaye jana aliachwa katika kikosi cha Dortmund kilichocheza dhidi ya Sporting Lisbon kutokana na sababu za ndani ya klabu.

39fef7c600000578-3898948-image-a-41_1478118961243
Aubameyang akiwa jukwaani akiangalia mechi dhidi ya Sporting Lisbon

Alitaraji kuanza katika mchezo huo wa klabu bingwa Ulaya lakini muda mchache kabla ya mechi jina lake halikuonekana katika kikosi na nafasi yake ilichukuliwa na Adrian Ramos ambaye alifunga goli pekee katika mechi hiyo.

Aubameyang ambaye hadi saivi amefunga magoli 10 katika mechi 13 katika msimu huu.

Baada ya mchezo kocha wa BVB Thomas Tuchel aliongea na waandishi alisema kuwa mchezaji huyo amefungiwa na klabu toka jumanne mpaka Alhamis (leo), lakini hakueleza sababu za zilizopelekea kifungo hicho

39ff09a700000578-3898948-image-a-49_1478120012034

Imeripotiwa kuwa Aubameyang alifungiwa juzi jumanne kwa sababu alikuwa akitumia simu yake wakati wa kikao cha timu kuelekea mechi ya jana, na pia sababu nyingine ya kufungiwa,mshambuliaji huyo jumatatu hii alienda katika sherehe ya rafiki zake huko nchini Italia bila ya kupata ruhusa kutoka klabuni.

Aubameyang amepewa onyo kali mbele ya wachezaji wenzake kwa kosa la kwenda kwenye Party huko Italia bila ya ruhusa na kuambiwa lazima awepo jukwaani katika mchezo dhidi ya Lisbon uliopigwa Iduna Park, ambapo alihudhuria na kuondoka dakika 10 kabla ya mchezo kuisha.

Mchezaji huyo atarejea uwanjani wikiendi hii katika mechi ya Bundesliga dhidi ya Hamburg, amethibitisha CEO wa BVB Joachim Watzke.

Facebook Comments
Share.

About Author