Home News SAMATTA AWAPA MZIGO HUU WACHEZAJI WENZAKE TAIFA STARS

SAMATTA AWAPA MZIGO HUU WACHEZAJI WENZAKE TAIFA STARS

1426
0

 

Nahodha wa timu ya Taifa Stars Mbwana Samatta amesema kuwa bado wana kazi ngumu mbele yao kuweza kushinda michezo miwili inayowakabili ili kuweza kufuzu kushiriki fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon).

Stars ipo kundi L ambalo linaongozwa na timu ya Uganda ambayo ina point kumi huku Stars ikiwa nafasi ya pili baada ya kukusanya point tano.

“Tumeshinda mchezo wetu wa kwanza ni jambo la kushukuru,ila tunapaswa tujue furaha yetu iwe ya kiasi hasa kwa kuwa safari ndo inaanza na tunapaswa kuongeza juhudi hasa kwa mechi zetu zinazofuata.

“Malengo yetu ni kuweza kushinda mechi zetu zinazofuata ili kuweza kufuzu kushiriki fainali kwa kuwa hizo ndizo hesabu zetu na tumedhamiria kufanya kweli kwa kuwa inawezekana”alisema.SALEHE JEMBE